Changamoto ni kwamba katika kumpata mchumba wa maisha huwa tunayapa matamanio yetu kipaumbele cha kwanza.
Baadae tunaanza kuteseka na kuhangaika katika mahusiano hayo, ambayo tunakuwa tumeyajenga juu ya vionjo vyetu vya hisia!
Njia rahisi na sahihi ya kufurahia maisha ya mahusiano katika ndoa ni kumtanguliza Mungu katika kumpata mchumba wako!
Tunapaswa kuhakikisha kila siku hatuchoki katika kumuomba Mungu na kumtumikia bila mawaa.
Kwenye sala zetu za kila siku, kabla na baada ya usingizi mnono, tunapaswa tuombe dua kwa Mwenyezi Mungu atuchagulie mchumba mwema wa maisha!
Bila ya kutaja jina, bila ya kuvuta taswira ya picha, bila ya kuvuta muonekano wa mtu na bila ya kuongozwa kwa vionjo vya hisia za kibinadamu tumtolee Mungu maombi ya kumpata mchumba mwema na bora wa maisha! AMEN!
TOA MAONI YAKO HAPA
BOFYA “LIKE” HAPO CHINI KUPATA HABARI ZETU..!!
